Heroin ni aina ya dawa ya kulevya itokanayo na mmea unaojulikana kama "Opium Poppy". Dawa hii hupumbaza mfumo wa fahamu.
Majina ya mitaani:Ina majina mengi kama unga, Brown sugar, Ngoma, Ubuyu, Mondo, Poda, Dume, Farasi n.k.
Heroin hutumika kwa watumiaji kwa kuvuta, au kunusa au kujidunga dawa hizi njia ambazo ni hatari kwa afya zao. Huongezwa sukari, kahawa, aspirini, panadol n.k. na kuufanya mchanganyiko huu kuwa hatari/sumu zaidi kwa watumiaji.
Madhara ya Heroin:. kuharibikiwa kwa mfumo wa fahamu.
. Kupata magonjwa ya moyo, ini, kifua na mapafu
. Kushuka kwa mapigo ya moyo.
. Kupata kizunguzungu, kichefuchefu, kutapika na kufunga choo.
.Hujenga hali ya uteja kwa haraka sana kuliko dawa zingine za kulevya.
.Utumiaji kwa njia ya kujidunga husababisha maambukizi ya virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine ya dawa kutokana na kushirikiana sindano na vifaa vingine.
.Dozi kubwa husababisha kifo.
Sheria inasemaje kuhusu Heroin:Kutumia, kuhamasisha, kuuza, kusafirisha, kuhifadhi au kujihusisha kwa namna yoyote ile na Heroin ni kosa la jinai. Adhabu kwa makosa hayo hufikia hadi kifungo cha maisha.
Kwa Ushauri na Msaada:. Nenda kwenye kituo cha ushauri au kituo cha afya kilicho karibu yako.
. Nenda
Mwenye kituo cha SHALOM CENTRE (kipo mwenge kituoni). Piga simu namba
0757 855858 ua 0655 287399. Tuma barua pepe:
mirium0280@gmail.com